Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88. Taarifa hizi zilitolewa Saa 9:45 asubuhi na Kardinali Kevin Farrell, Camerlengo wa Baraza la Kitume.
Papa alilazwa katika Hospitali ya Agostino Gemelli Polyclinic mnamo Ijumaa, Februari 14, 2025, baada ya kuugua ugonjwa wa bronchitis kwa siku kadhaa.Baada ya siku 38 hospitalini, marehemu Papa alirejea katika makazi yake ya Vatican kwenye Casa Santa Marta ili kuendelea na matibabu.
Papa Francis mara kwa mara aliugua magonjwa ya kupumua, hali iliyompelekea kutohudhuria ziara iliyopangwa katika Umoja wa Falme za Kiarabu mnamo Novemba 2023 kutokana na mafua na kuvimba kwa mapafu.
Mnamo Aprili 2024, Hayati Papa Francis aliidhinisha toleo jipya la kitabu cha kiliturujia kwa ajili ya ibada za mazishi ya papa, ambalo litaongoza Misa ya mazishi ambayo bado haijatangazwa.
At 9:45 AM on Easter Monday, Cardinal Kevin Farrell, Camerlengo of the Apostolic Chamber, spoke these words at the Casa Santa Marta:
“Dearest brothers and sisters, with deep sorrow I must announce the death of our Holy Father Francis. At 7:35 this morning, the Bishop of Rome,…
— Vatican News (@VaticanNews) April 21, 2025