Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah ameibua shutuma dhidi ya aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta akidai kuwa yeye ndiye aliyesababisha mgawanyiko wa viongozi kuhusu ripoti ya mazungumzo ya kitaifa.

Hii ni baada ya aliyekuwa mgombea mwenza wa urais wa Azimio la Umoja Martha Karua na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa kupinga mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (NADCO), wakiteta kuwa walishindwa kushughulikia masuala muhimu.

Kupitia mtandao wake wa X, Ichung’wah alidai kuwa Bw. Kenyatta amekuwa akiingilia juhudi zinazofanywa na serikali katika kuleta mageuzi katika taifa. Kamati hiyo ya mazungumzo ilisema kuwa walishindwa kufikia mwafaka kuhusu Ushuru wa Nyumba wenye utata pamoja na kupunguzwa kwa VAT ya mafuta kutoka 16% hadi 8%.

November 27, 2023