Mawaziri Kithure Kindiki wa usalama wa ndani, Ezekiel Machogu wa Elimu pamoja na Susan Nakhumicha wa Afya wameorodheshwa kama mawaziri wanaotekeleza majukumu yao kikamilifu katika utafiti wa hivi majuzi.

Utafiti huo, uliotolewa Alhamisi na kampuni ya utafiti ya TIFA, ulimweka waziri Kindiki juu ya orodha hiyo akiwa na asilimia 34.

Hata hivyo, asilimia 40 ya waliohojiwa katika utafiti huo walitoa maoni kwamba hakukuwa na waziri anayefanya vyema katika Baraza la Mawaziri.

TIFA ilifanya mahojiano katika kanda 9 nchini zikiwemo Central Rift, Pwani, Lower Eastern, Mt Kenya, Nairobi, Northern, Nyanza, South Rift, Western. Jumla ya watu 1,530 waliohojiwa walihojiwa kati ya Juni 24 na Juni 30, 2023.

July 13, 2023