Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu nchini (KNCHR) imeelezea wasiwasi wake kuhusu mauaji ya kiholela na visa vya watu kutoweka nchini.
Mwenyekiti wa tume hiyo Roseline Odede amesema matukio hayo yameendelea kukiuka na kutishia haki ya kuishi na kuongeza kuwa katika baadhi ya matukio uchunguzi umedaiwa kuelekeza vyombo vya usalama na ushirikishwaji wa wahusika wasio wa serikali wakiwemo majambazi.
Kulingana na ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa hii leo, kesi 22 za mauaji ya kiholela na kesi 9 za kutoweka kwa lazima zilirekodiwa kati ya Januari 2022 hadi Juni 2023 huku wengi wa waathiriwa wakiwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35.
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa mnamo Septemba mwaka jana, miili 39 iligunduliwa katika Mto Yala na Msitu wa Aberdare mnamo Machi 2023.
FULL PRESS STATEMENT ON THE STATE OF HUMAN RIGHTS IN KENYA. pic.twitter.com/D4ybpgWxKB
— KNCHR (@HakiKNCHR) November 22, 2023
— KNCHR (@HakiKNCHR) November 22, 2023
— KNCHR (@HakiKNCHR) November 22, 2023