Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini (KNEC) limezungumzia baadhi ya hitilafu zilizoripotiwa na baadhi ya watahiniwa katika matokeo ya hivi punde ya KCPE 2023.
Baraza hilo katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari siku ya Jumamosi lilibainisha kuwa limepokea malalamishi kufuatia baadhi ya makosa ya matokeo.
Kulingana na barazahilo, matokeo yote kwenye tovuti yake yalikuwa sahihi, hivyo makosa hayo yaliathiri tu baadhi ya watahiniwa waliopata matokeo yao kupitia SMS. Hata hivyo baraza hilo limewahakikishia watahiniwa kuwa limezungumza na mtoa huduma wa SMS na wameahidi kurekebisha makosa hayo.
Press statement on 2023 KCPE examination results queries. pic.twitter.com/Sm95D4RRV4
— KNEC (@KNECKenya) November 25, 2023