BY ISAYA BURUGU,07.NOV,2022-Wakuu wa nchi na serikali wanatarajiwa kutoa hoja zao kuhusu hatua za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wakati wa Mkutano wa COP27 nchini Misri.
Awamu ya kwanza ya mkutano huo itajumuisha hotuba za viongozi kutoka nchi zenye uchumi mkubwazinazozalisha mafuta na pia kutoka nchi zinazoendelea zilizoathirika zaidi na athari za ongezeko la joto duniani.
Mataifa tajiri zaidi yanapaswa kuelezea mipango yao ya kupunguza uzalishaji wa kaboni.Nchi maskini zimekaribisha uwezekano wa mjadala wa kuanzisha hazina ya fidia, huku suala hilo likijumuishwa kwenye ajenda kwa mara ya kwanza tangu Umoja wa Mataifa kupitisha mkataba wake wa mabadiliko ya tabianchi.
Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, Simon Stiell, alisema kwamba bado kuna nafasi ya kupunguza ongezeko la joto duniani linalochangiwa na viwanda.Rias Wiliam Ruto anatarajiwa kuwsilisha ujumbe wa mataiafa ya Afrika kwenye kongamano hilo.