BY ISAYA BURUGU,6TH SEPT 2023-Serikali imepitisha Azimio la Nairobi kutenga fedha zitakazoelekezwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Viongozi wameahidi kuchangisha anagalau dola bilioni mia moja kufadhili miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Katika kongamano la Afrika kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi,viongozi hao pia wameapa kutumia mkutano mkuu wa umoja wa mataiafa ujao na kongamano la COP28 kushinikiza mageuzi kwenye mifumo mikuu ya mataiafa makubwa yaliyostawi katika juhudi za kuhakikisha kuwa rasilimali za kutosha zinapatikana kuyawezesha mataiaya ya Afrika kufanikiwa katika juhudi za kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Taarifa ya viongozi hao imesomwa na rais Wiliam Ruto katika kiko cha Pamoja na wanahabari.