BY ISAYA BURUGU 23RD DEC,2022-Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini imesema inalaani hatua ya Korea Kaskazini kupeleka silaha kwa kampuni binafsi ya kijeshi ya Urusi ya Wagner Group. Wizara hiyo imesema leo pia inaunga mkono shinikizo la Marekani kuliwasilisha suala hilo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hapo jana, msemaji wa baraza la usalama la Marekani John Kirby alisema Korea Kaskazini imekamilisha upelekaji wa awali wa silaha kwa kundi la Wagner Group ili kulisaidia kuimarisha vikosi vya Urusi nchini Ukraine. Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imekanusha taarifa kwamba imeipatia Urusi silaha ikisema kuwa sio za msingi. Na badala yake nchi hiyo imeishutumu Marekani kwa kuipatia Ukraine silaha za kivita. Taarifa ya wizara hiyo hata hivyo, haijalitaja popote kundi la Wagner.