BY ISAYA BURUGU,11TH MARCH,2023-Lori lililokuwa limepakiwa kwenye barabara ya Kakamega-Kisumu karibu na makao makuu ya serikali ya kaunti ya Kakamega imebingiria na kuangukia magari mawili yaliyokuwa yamepakiwa karibu na makao makuu ya kaunti hiyo kabla ya kugonga jengo lililo na afisi za gavana.
Lori hilo lililokuwa na nembo ya maduka ya jumla ya khetias lilikuwa limebeba bidhaa za duka.Aliyeshuhudia amesema dereva wa lori hilo hakuwa ndani wakati ajali hiyo ilipotokea akiongeza kuwa huenda lori hilo lilibingiria kutokana na uzito wa mizigo lililokuwa limebabe.
Hata haikubainika haraka iwapo dereva alikuwa ametumia breki.Askari wa kaunti ya lkakamega wamelaumiwa kwa kuyaruhusu magari kugezwa kwenye maeneo yasiyohitajika.