BY ISAYA BURUGU,29TH APRIL,2023-Luteni generali Francis Omondi Ogolla na luteni generali Jonah Maina Mwangi wameapishwa rasmi hivi leo kama mkuu wa majeshi na naibu wake mtawalia katika hafla iliyoandaliwa katika ikulu ya Nairobi.Ogolla anachukua mahala pa generali Robert Kariuki Kibochi ambaye muda wake wa kuhudumu umefikia mwisho.Generali Ogolla hadi wakati wa kuteuliwa kwake kama mkuu wa majeshi na rais Wiliamu Ruto alikuwa akihudumu kama naibu mkuu wa majeshi .
Generali Kibochi kwa mjibu wa arifa kutoka kwa wizara ya ulinzi anaondoka baada ya kuhudumu kwenye idara ya kijeshi kwa miaka 44.Rais Ruto katika mabadiliko hayo pia amempandisha ngazi Generali Said Farah kuwa naibu chanzela wa chuo kikuu cha ulinzi nchini .
Brigedia David Kipkemboi Keter alipandishwa ngazi kuwa meja generali na kuteuliwa naibu mkuu wa majeshi kitengo cha rasilimali watu na mipango.Rais pia amempandisha ngazi brigedia Stephen James Mutuku kuwa meja generali na kumteua kama mfanyikazi wa hadhi ya juu atakaye toa maagizo kwenye jeshi katika chuo anua cha kitaifa cha ulinzi.
Wakati huo huo rais Wiliam Ruto amemtaka mkuu mpya wa majeshi Luteni generali Francis Omondi Ogolla kulihudumia taifa katika wadhifa huo wake mpya kwa taadhima ya hali ya juu.Rais akisema kuwa ana Imani kuwa Ogolla atatekeleza wajibu wake kama inavyohitajika.Amemtaka kuhakikisha kuwa maadili mema na kitaluma aliyoyapata kwenye jeshi yanaendelea jinsi yalivyo chini ya utawala wake..