BY ISAYA BURUGU ,1ST DEC 2022-Kenya inaungana na ulimwengu leo kuadhimisha siku ya ukimwi duniani huku maambukizi ya virusi vya HIV na ugonjwa wa Ukimwi yakiripotiwa kuongezeka kwa mara ya kwanza nchini katika muda wa miaka kumi iliyopita.Haya ni kwa mjibu wa ripoti.
Ripoti hiyo ya maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa Ukimwi duniani mwaka itakayozinduliwa leo inadokeza kuwa Kenya ilirekodi ongezeko la maambukizi mapaya ya HIV kwa mara ya akwanza ndani ya miaka kumi kwa Zaidi ya visa 2000 kutoka visa alfu 32,025 hadi kufikia visa 34, 540.
Katika kipindi cha mwaka jana pekee Kenya ilisajili visa vipya vya maambukizi ya HIV vipatavyo 34,540 HIV .
Ripoti hiyo inahusisha hali hiyo na maambukizi mapaya miongoni mwa Watoto ,vijana wanaobalehe na watu wachanga sawa na upungufu wa dawa za kukabili makali ya ugonjwa wa Ukimwi.
Ripoti hiyo kwa jina it is a race against time iliyoandaliwa na baraza la kitaifa la kudhibiti magonjwa yaani the National Syndemic Disease Control Council imefichua kuwa visa vipya vya maambukizi ya virusi vya HIV Vipatavyo 34,540 vilisajiliwa huku asilimia 70 kati ya visa hivyo jumla ya 20,505 vikisajiliwa miongoni mwa wanawake na wasichana .