Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi (NPSC) imechapisha majina nane ya maafisa walio na nia ya kutwaa nyadhifa za Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kitaifa (NPS) na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi ya Utawala (APS).
Nafasi hizo ziliachwa wazi wiki jana kufuatia kuteuliwa kwa aliyekuwa Naibu Inspekta Jenerali wa NPS Douglas Kanja kama Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini na kutumwa tena kwa aliyekuwa naibu Inspekta Jenerali wa Polisi ya APS Noor Gabow kwa Idara ya Utumishi wa Umma.
SOMA PIA : Polisi Wapiga Marufuku Maandamano Katikati Mwa Jiji la Nairobi.
Walioteuliwa kuwania nafasi ya Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kitaifa ni:
- George Adero Sedah
- Eliud Kipkoech Lagat
- Tom Mboya Odero
- Dkt Vincent Kinas Makokha
Kwa upande mwingine, walioteuliwa kuwania wadhifa wa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi wa Utawala ni:
- Gilbert Masengeli
- Margaret Nyambura Karanja
- James Mukuha Kamau
- Dkt Masoud Mwinyi
Zoezi la kuwapiga msasa walioteuliwa kutwaa nyadhifa za Naibu Inspekta Jenerali litaandaliwa Jumatatu ijayo, Julai 22, 2024, kuanzia saa 9:30 asubuhi.
1/
The National Police Service Commission today kicked off the exercise of shortlisting candidates for the position of Deputy Inspector General (D.I.G) of Kenya Police Service and Administration Police Service respectively. @NPSOfficial_KE @PoliceKE @APSKenya pic.twitter.com/NJmLWBNMfn— National Police Service Commission – Kenya (@NPSC_KE) July 18, 2024