Maafisa wa polisi sasa hawataruhusiwa kuhudumu katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitatu.
Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ambaye amesema kwamba wizara hiyo imeanzisha juhudi za kuhakikisha kwamba maafisa waliohuduma katika kituo kimoja kwa muda wanapata uhamisho, kama mojawapo ya njia za kuimarisha utendakazi katika sekta ya huduma za polisi.
Kindiki alikua akizungumza katika kikao cha Bunge alipokua anajibu maswali yaliyoibuliwa na wabunge kutwa ya leo. Waziri Kindiki amekuwa Waziri wa kwanza katika utawala wa Rais William Ruto kufika mbele ya kikao cha bunge kujibu maswali yaliyoulizwa na wabunge.
Kuhusiana na suala la mauaji ya kiholela yanayotekelezw ana maafisa wa polisi, Waziri huyo ameeleza kwamba maafisa waliohusika katika kesi za aina hii wanaendelea kuchunguzwa na idara husika, huku akisisitiza kwamba wizara hiyo haita mtetea yeyote atakayetumia silaha yake kinyume cha sheria.
As a policy, we will ensure that no police officer, of whatever rank, will serve in one police station for more than three years. pic.twitter.com/HpXyKjd9W4
— Kithure Kindiki (@KindikiKithure) April 12, 2023