BY ISAYA BURUGU ,19TH DEC 2022-Maafisa wa polisi wa DCI wamemkatama mwanname mmoja wa miaka 26 kuhusiana na jaribio la mauaji yam toto Juniour Sagini kule marani kitutu chache kasikiani kaunti ya Kisii.Kwa mjibu wa polisi ni kwamba mwanamme huyo Alex Maina Ochogo ndie mshukiwa mkuu wa jaribio la maujai yam toto huyo mwenye umri wa miaka mitatu kwa kumngoa macho.OChogo anawasilishwa mahakamani huko kisii kukabiliana na kosa hilo la kujaribu kumua mtoto huyo.
Wakati huo huo Mama wa mtoto Junior Sagini mwenye umri wa miaka 3 aliyevamiwa na macho yake kung’olewa na watu wasiojulikana huko Kisii anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi leo.
Mama huyo kwa jina Maureen Nyaboke, alijitokeza kwa mara ya kwanza jana jumapili tangu kisa hicho kutokea .Kwa mjibu wa rekodi za polisi ni kwamba Nyaboke mwenye umri wa miaka 28 alimwacha mtoto huyo pmoja na mtoto msichana wa miaka saba chini ya uangalizi wa babake na nyanyake.
Anaripotiwa kuenda kufanya kazi kama mhudumu wa baa eneo Nyamakoroto, kaunti ya Nyamira wakati kisa hicho cha kuhuzunisha kilipotokea jumatano wiki iliyopita.Ni mara ya kwanza mamake Sagini alikuwa akitembelea hospitali ya macho ya Kisii ambapo mtoto wake amekuwa amelazwa.
Wakati Nyaboke alipokuwa akijiandaa kuondoka hospitalini maafisa wa polisi walifika na kumtia mbaroni na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Rioma kuhojiwa.Mama huyo amekesha korokoroni usiku wa leo huku akitarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kumtelekeza mwanawe.