BY ISAYA BURUGU 25TH NOV 2023-Maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wamewakamata wafanyikazi wanne wa Wells Fargo wanaoaminika kusaidia katika wizi wa zaidi ya shilingi milioni Ksh.94 wa Quickmart uliotokea wiki mbili zilizopita.

kukamatwa kwa wanne hao , yaani; Joel Oyuchi Mweseli, Harrison Mugendi Njeru, Caleb Ouma Okinyi na Ronald Ouma Oluu, kunajiri huku makachero kuwawinda watu wawili ambao pia wameajiriwa na kampuni ya ulinzi ya usafirishaji ya wells fargo wanaoaminika kuwa  wapangaji  wakuu wa wizi huo.

Mweseli anashikilia nafasi ya mpanga mipango ndani ya Wells Fargo ilhali Njeru ndiye mkuu wa madereva; Okinyi anahudumu kama msimamizi wa magari , huku Oluu akiwa na jukumu la kusimamia wasimamizi  wa wafanyakazi. Wote watafikishwa mahakamani Jumatatu.

Kufikia sasa, washukiwa wanane wamekamatwa kuhusiana na wizi huo baada ya DCI, Novemba 12, kuwakamata watu wanne wanaohusishwa na wizi huo.

 

 

November 25, 2023