Huku ulimwengu unapoadhimisha siku ya ukimwi duniani hivi leo, wakaazi wa kaunti ya Narok wamepongeza juhudi zinazofanywa na serikali katika  kuwasaidia waathiriwa wa ugonjwa huo.

Kwa mjibu wa  wakaazi wa kaunti hii waliozungumza na idhaa ya radio Osotua,wamesifia serikali ya kitaiafa  kwa kuwapa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi usaidizi wanaohitaji ukiwemo mafunzo ya jinsi ya kuishi na kutunza afya zao na kuwasilisha dawa za kukabilina na makali ya ugonjwa huo hospitalini kwa wakati ufaao.

Aidha wakaazi hao wamewahimiza wanaoishi na virusi vya ukiwmi kufuata mawaidha ya daktari kila wakati ili waweze kuishi vyema. Katika Kaunti ya Narok Idadi ya maambukizi ya virusi vya HIV ni asilimia 3.1 ambayo ni ya chini ikilinganishwa na kiwango cha maambukizi kitaifa ambayo ni asilimia 5.9 kwa mjibu wa tathmini ya kitaifa ya maambukizi ya ugonjwa huo ya mwaka 2015.

Aidha Kote nchini maambukizi ya HIV yamepungua kwa 78% tangu 2013 huku vifo kutokana na maambukizi vikiendelea kuripotiwa. Jumla ya Watu milioni 1.4 wanaishi na virusi hivyo nchini.

Wakati huo huo waziri wa Afya Susan Nakhumicha Wafula ameunga mkono jamii kwa jukumu lao muhimu ambalo linalenga katika kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.

Akizungumza katika Kaunti ya Meru wakati wa kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, Nakhumicha amepongeza jamii kwa kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na usambazaji wa virusi vya UKIMWI tangu kuanza kwa ugonjwa huu zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Hata hivyo waziri huyo ametetea kubuniwa kwa mamlaka ya afya ya jamii akisema kuwa mamlaka hiyo itahakikisha  kila mmoja anapata matibabu.

December 1, 2023