Ukimwi

Maambukizi ya virusi vya Ukimwi yamepungua kutoka asilimia 5.6 hadi asilimia 1.8 katika Kaunti ya Narok katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Gavana wa Kaunti ya Narok, Patrick Ntutu, alitoa takwimu hizi siku ya Jumatatu 13.01.2025 wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku nne ya kutoa mwelekeo wa kumaliza ugonjwa wa Ukimwi.

Warsha hiyo iliyoandaliwa katika hoteli ya Mara Frontier Mjini Narok, imewaleta pamoja washiriki kutoka nchi sita za mabara matatu duniani, zikiwemo Kenya, Uganda, Nigeria, Marekani na Ufilipino. Gavana Ntutu alisisitiza kuwa juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi zinaendelea, huku akibainisha mafanikio makubwa katika kupunguza maambukizi, hasa kwa watoto.

Kauli ya gavana imeungwa mkono na Dr. Patricia Angata, mkurugenzi wa shirika la Henry Junction Foundation kutoka Marekani, ambaye alisema shirika lake linashirikiana na serikali ya Narok na washikadau wengine kuhakikisha maambukizi mapya yanatokomezwa kabisa.

Mary Smith, naibu mkurugenzi wa shirika la Global Health, aliongeza kuwa serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na serikali ya Kenya kuboresha mbinu za kupunguza magonjwa ya kuambukizana na kuimarisha afya ya umma.

January 14, 2025

Leave a Comment