Kinara wa upinzani Raila Odinga amesisitiza kwamba shughuli za uasi zitaendelea kote nchini kuanzia siku ya Ijumaa wiki hii, kama njia mojawapo ya kupinga uongozi wa serikali.
Odinga alitoa taarifa hiyo kwa umma leo alasiri na kueleza kuwa muungano huo unaendeleza shughuli zake kwa mujibu wa sheria na katiba ya taifa. Aidha, amesisitiza kuwa hawatatishwa na yeyote katika kutekeleza malengo yao. Kinara huyo wa Muungano wa Azimio la Umoja amewaomba wafuasi wake kujitokeza katika uwanja wa Kamukunji na maeneo mengine ya taifa ili kushiriki katika maandamano hayo.
Wakati huo huo, Odinga amepongeza uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa jana, ambapo nyadhifa za mawaziri waratibu zilitangazwa kuwa zilizoidhinishwa kinyume cha sheria. Odinga ameeleza kuwa mahakama imefuata utaratibu wa kisheria katika utekelezaji wa majukumu yake.
AZIMIO STATEMENT July 4, 2023
Ladies and Gentlemen,We gather here today because THE PEOPLE HAVE HAD ENOUGH. There comes a time when being taken for granted becomes unbearable. There comes a time when being treated as fools becomes intolerable. That time has come.
Henceforth,… pic.twitter.com/TvF3wAc6T3
— Azimio TV (@AzimioTv) July 4, 2023