BY ISAYA BURUGU 3RD JULY,2023-Macho yote hivi leo yanaelekezewa mahakama kuu wakati mahakama hiyo ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa makatibu wakuu wasimamzi 50. Chama cha wanasheria nchini LSK na shirika la katiba institute ilikwenda mahakamani kuzuia mchakato huo kwa misingi kuwa unakiuka katiba.
Mashirika hayo mawili yalidai kuwa katiba yam waka 2010 haijabuni nafasi za makatibu hao nah atua ya kuwachagua itachangaia mzigo mzito kwa mwannachi mlipa ushuru ambaye atalamizika kugharamia mishahara yao.Ni ombi lililokubaliwa na mahakama iliyositisha mpango huo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.
LSK na Katiba institute pia yanadai kuwa hatua ya rais kuwateua makatibu hao wakuu wasimamizi 50 kinyume na 23 wanaopendekezwa imechangia kubuni nafasi 27 zilizo kinyume cha katiba.