BY ISAYA BURUGU 7TH SEPT,2023-Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC)  imetoa ilani kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa hivi leo  Alhamisi.Katika taarifa yake, kampuni hiyo ilitangaza kuwa maeneo kadhaa katika kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Kiambu, Machakos, Kisii, Homa Bay, Nyeri na Meru.

Katika kaunti ya Kiambu,Toll Station, Murera Coffee, Mugutha, Ruiru Golf Club, Titanic, Courtesy Beach, Green Ridge, Murera Primary, Tumaini Catholic Church, Mugutha One Four, Mukuyu Road, Judea Estate, Mugutha Police, Neema Estate, Riverline, Estate, Damridge Estate, Ruera Dam, Makaburi Village, Wakariuki na majirani wake ni baadhi ya maeneo ambayo yataathirika kuanzia saa tatu hadi saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kithimani, Ngoliba, Kabaa, Kenyatta Farm, Delmonte Engel, NYS Yata na majirani wake katika kaunti ya Machakos pia yataathiriwa.Katika kaunti ya Nyeri; Kiawarigi, Gitunduti,Kiamuturi, Gatunguru, Kiriti T. Factory na maeneo ambayo yanazingira yaliyotajwa yatakuwa bila stima kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.Eneo la Nyanchwe na sehemu za mji wa Kisii katika kaunti ya Kisii pia yataathiriwa kati ya saa tatu asubuhi na saa nane mchana.

Katika kaunti ya Homa Bay, baadhi ya maeneo katika mji wa Homa Bay, Rangwe na Homa Hills yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Vilevile. Kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni, baadhi ya sehemu za maeneo ya Embori, Kikwetu, Kisima, PJ Dave Farms na Homegrown katika kaunti ya Meru pia hayatakuwa na umeme.

 

September 7, 2023