Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu iwapo itaondoa kesi ya ulaghai inayomkabili Naibu Rais Rigathi Gachagua na watu wengine tisa. Hii ni baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kutaka kesi hiyo iondolewe kwa misingi kuwa uchunguzi wa kesi hiyo haujakamilika.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, itakuwa ni upendeleo kwa kesi hiyo kuendelea kama ilivyo.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji alimweleza hakimu wa mahakama kuwa ushahidi haukidhi kizingiti kinachohitajika kufikia kufanikiwa kwa kesi hiyo. Haji anataka kesi hiyo iondolewe chini ya kifungu cha 87 A cha kanuni za makosa ya jinai.Kifungu hicho kinamruhusu DPP kuwakamata na kuwafungulia mashtaka watuhumiwa kwa kosa hilohilo mara watakapopata ushahidi mpya.