Mahakama kuu imeamua kuwa uteuzi wa makatibu wakuu ni kinyume cha katiba.
Akitoa uamuzi huo, jaji Hedwig Ongundi amesema kuwa haikuwa nia ya waundaji wa Katiba kuwa makatibu wakuu 50 kama wasaidizi wa mawaziri 22.
Ameongeza kuwa tume ya kuwaajiri wafanyakazi wa umma PSC haikufuata sheria ikizingatiwa kwamba haikukusanya maoni ya wakenya kuhusu uteuzi huo.
Makatibu hao waliteuliwa na rais William Ruto mnamo machi mwaka huu na kukula kiapo mwezi huohuo.
Itakumbukwa kwamba Chama cha wanasheria nchini LSK na shirika la katiba institute lilikwenda mahakamani kuzuia mchakato huo kwa misingi kuwa unakiuka katiba.
Mashirika hayo mawili yalidai kuwa katiba ya mwaka 2010 haijabuni nafasi za makatibu hao na hatua ya kuwachagua itachangaia mzigo mzito kwa mwananchi mlipa ushuru ambaye atalamizika kugharamia mishahara yao.
LSK na Katiba institute pia yalidai kuwa hatua ya rais kuwateua makatibu hao wakuu wasimamizi 50 kinyume na 23 wanaopendekezwa imechangia kubuni nafasi 27 zilizo kinyume cha katiba.