BY ISAYA BURUGU 6TH SEPT 2023-Mahakama kuu nchini imefutilia mbali uteuzi wa Alice Kering kama mwakilishi wadi mteule kwenye bunge la kaunti ya Narok.
Mahakama hiyo kupitia jaji Francis Gikonyo imempa ushindi Josphine Seneyio Torome aliyewasilisha kesi ya kupinga uteuzi huo wa Alice Kering’ ambaye aliteuliwa na chama cha Jubilee kuwakilisha maslahi ya akina mama kwenye bunge hilo kwa madai kwamba sio mwanachama wa jubilee na sio mpiga kura wala mkaazi wa Narok.
Ilikuwa shangwe na nderemo kwa wakaazi wa Narok, jamaa na marafiki wa Josphine Seneyio Torome baada ya mahakama kuu kumpa ushindi huku ikifutilia mbali uteuzi wa Alice Kering’ aliyeteuliwa na chama cha jubilee kuwakilisha maslahi ya akina mama kwenye bunge la kaunti ya Narok baada ya uchaguzi mkuu uliopita.
Mahakama hiyo ikiunga mkono uamuzi uliotolewa na mahakama kuu ya Narok kwamba Bi. Kering sio mwanachama wa jubilee, mkaazi ama mpiga kura katika kaunti ya Narok na kisheria anapaswa kuwa mwanachama wa chama hicho na mpiga kura na vile vile mkaazi wa Narok ili aweze kuteuliwa kama mwakilishi wadi kwenye bunge la kaunti ya Narok.
wakili wa Seneyio Torome akiitaka tume ya IEBC kuchapisha rasmi jina la Seneyio Torome kama mwakilishi wadi mteule kwenye bunge la kaunti ya Narok.Ni ushindi ambao umepokelewa kwa furaha na Josphine Seneyio Torome..