Mahakama kuu nchini imesitisha kwa muda utekelezaji wa mswada wa fedha wa mwaka 2023 kwa kipindi cha juma moja, ili kupisha kumalizika kwa kesi iliyowasilishwa na seneta wa Busia Okiya Omtatah, ikipinga baadhi ya vipengee vilivyo kwenye mswada huo.
Katika kesi yake Omtatah amesema kwamba baadhi ya vipengee havina uhusiano wowote na maswala ya ushuru, huku akitaja kwamba vingine havijazingatia sheria na hivyo kufanya ngumu kazi ya seneti kuwalinda wakenya dhidi ya Dhuluma. Jaji Mugure Thande alitoa uamuzi wa kusitisha kuanza kutekelezwa kwa sheria hiyo kuanzia hapo kesho, hadi tarehe 5 mwezi Julai Kesi hii itakaposikilizwa na maagizo zaidi kutolewa. Omtatah sasa anaitaka mahakama kufuta baadhi ya vipengee kwenye mswada huo.