BY ISAYA BURUGU 24TH OCT 2023-Mahakama kuu hivi leo  imetowa uwamuzi wa kurefusha amri ya kuizuia serikali  kutowapeleka mamia ya maafisa wa polisi nchini Haiti, kupitia mpango unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa kwa lengo la kuleta amani katika taifa hilo la visiwa vya Caribbean.

Hakimu Enock Mwita amesema kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa wa upinzani Ekuru Aukot kuhusiana na suala hilo itasikilizwa mnamo Novemba 9.

Uamuzi huo wa mahakama unakuja siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kwamba hali ya usalama nchini Haiti, ambapo magenge ya uhalifu yanadhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo, imezidi kuwa mbaya huku uhalifu ukiweka rekodi kwa kufikia viwango vya juu zaidi.

Kujihusisha kwa Kenya katika mpango huo wa kuwapaleka polisi wake nchini Haiti kumetiliwa mashaka na wengi humu nchini huku wengi wakijiuliza maswali kuhusiana na busara iliyotumika kuidhinisha mpango hatari kama huo.

 

 

 

 

October 24, 2023