Mahakama ya Rufaa nchini imeongeza muda wa kutoa uamuzi kuhusu kesi inayohusu ada ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu, hivyo kuwalazimu Wakenya wanaotozwa ada hizo kusubiri kwa muda zaidi kujua hatma ya malipo yao. Uamuzi huo umesogezwa hadi tarehe 26 mwezi huu.

Mahakama hiyo, hata hivyo, haikusitisha ukusanyaji wa ada hizo licha ya uamuzi wa mahakama ya juu nchini kutangaza ada hizo kuwa kinyume cha sheria. Awali, mahakama ya juu ilikuwa imetoa muda hadi tarehe 10 kwa serikali kuendelea kuwatoza wafanyakazi ada hizo. Hata hivyo, muda huo umeongezwa kwa siku 16 zaidi kuanzia leo.

Taarifa hii inakuja wakati ambapo kuna mizozano kati ya serikali na idara ya mahakama. Rais William Ruto na viongozi wengine wametoa shutuma dhidi ya idara ya mahakama, wakiituhumu kwa kuhujumu utendakazi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya serikali.

 

 

January 4, 2024