Mahakama ya Rufaa ya Nyeri mapema hii leo ilikataa kusimamisha Bunge la Kaunti ya Meru kujadili hoja ya kumtimua Gavana Kawira Mwangaza.
Gavana huyo aliwalisilisha ombi Mahakamani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Meru dhidi yake wa kusitisha bunge hilo kujadili kuhusu kuondolewa kwake afisini, akisema suala hilo si la dharura.
Jaji Aggrey Muchelule na majaji wengine wawili waliahirisha uamuzi wa kesi hiyo hadi Oktoba 27. Marius Maranya, mmoja wa mawakili wanaowakilisha bunge la kaunti ya Meru alidai kuwa mahakama hiyo ikiwa chombo cha kikatiba haikuwa na mamlaka ya kuzuia bunge kutekeleza majukumu yake.
Baada ya uamuzi huo, bunge hilo liliendelea na kujadili hoja ya kumbandua gavana Mwangaza,hii ikiwa mara ya pili kwa hoja kama hiyo kuwasilishwa dhidi yake.