Mahakama ya Rufaa imekataa kuondoa agizo la Mahakama Kuu la kusimamisha Sheria ya Fedha ya 2023.

Mahakama hiyo iliagiza wahusika kufika kutoa uamuzi Julai 28, ambapo mahakama itaamua iwapo maagizo ya utekelezaji wa Sheria hiyo yataondolewa, kama alivyotaka Waziri wa Hazina ya kitaifa Prof. Njuguna Ndung’u.

Mnamo Julai 18, Jaji Mkuu Martha Koome aliteua jaji wa Mahakama Kuu David Majanja (jaji msimamizi), jaji Christine Meoli na Jaji Lawrence Mugambi kusikiliza na kuamua kesi kuhusu mswada huo.

Katika kesi hiyo, seneta wa Busia Okiya Omtatah na wengine walielekea kortini kupinga Sheria ya Fedha ya 2023, wakisema kuwa ni kinyume cha katiba.

July 20, 2023