Mahakama ya Rufaa imesitisha maagizo yaliyotolewa na Mahakama Kuu yaliyosimamisha utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya ya Jamii ya mwaka 2023.
Jopo la majaji watatu, linalojumuisha Majaji Patrick Kiage, Pauline Nyamweya, na Grace Ngenye pia waliondoa maagizo ya kuzuia utekelezaji wa Sheria ya Afya ya Msingi, 2023, na Sheria ya Afya ya Kidijitali, 2023.
Katika uamuzi huo uliotolewa hii leo, majaji hao walisema kwamba kesi inayoendelea mahakamani ni hatari kwa haki za kiafya za raia wengi ambao hawashiriki katika suala linaloendelea.
Hata hivyo, sehemu kadhaa za Sheria ya Bima ya Afya ya Jamii zimesalia kusimamishwa kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa.
Sheria hiyo ya Bima ya Afya ya Jamii imepaniwa kuchukua nafasi ya Bima ya Afya ya sasa NHIF na kuanzisha hazina tatu mpya.