BY ISAYA BURUGU 8TH SEPT 2023-Mahakama ya Juu Zaidi imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah na wengine kupinga kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha, 2023.

Katika uamuzi uliotolewa leo , mahakama ya upeo  iliamua kwamba haina mamlaka ya kushughulikia  rufaa hiyo, na kuongeza kuwa haijashawishika kuwa uamuzi wa  Mahakama ya rufaa uliotupilia mbali ombi la Omtahatah ulisababisha ukosefu wa haki ili kudhibitisha mamlaka yake.

Zaidi ya hayo, mahakama imetupilia mbali mawasilisho yote yaliyowasilishwa na waombaji ikisema kuwa yaliwasilishwa nje ya muda.Majibu pia yalitolewa.

 

 

 

 

 

 

 

September 8, 2023