kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, ameeleza kwamba maandamano yaliyoratibiwa kuandaliwa siku ya Jumatatu juma lijalo yataendelea kama yalivyoratibiwa.

Katika kikao na waandishi wa habari alasiri ya Leo, Odinga amesema kwamba muungano huo umepata kufahamu kuhusu njama ya viongozi wa serikali kuwatumia vijana kusababisha maafa, ili kuvuta jicho la mahakama ya kimataifa.

Kuhusiana na wito wa majadiliano kutoka kwa viongozi wa kidini, Odinga amewataka viongozi na mashirika ya kidini kuendeleza wito wa haki badala ya kuwarai kuingia katika mazungumzo.

Kwa upande mwingine, Rais William Ruto amewataka viongozi wa Upinzani kusitisha maandamano yao, na pia kuyakubali matokao ya uchaguzi mkuu uliopita, ili kuliruhusu taifa kusonga mbele.

Rais aliyasema haya katika kaunti ya Kisii, baada yake kuanza ziara rasmi ya siku tatu, ambapo anatarajiwa kuendeleza msururu wa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kaunti hiyo na pia kaunti Jirani ya Nyamira.

Rais aliwaahidi wananchi kuwa serikali inatekeleza kila liwezekanalo ili kushusha gharama ya Maisha nchini.

March 23, 2023