BY ISAYA BURUGU 22ND DEC 2022-Rais William Ruto amemteua aliyekuwa jaji mkuu David Maraga kama mwenyekiti wa jopokazi litakalotathmini jinsi ya kuimarisha mazingira ya utendakazi kwa polisi na maafisa wa magereza.Maraga atasaidiwa na Carole Karuiki kwenye jopokazi hilo lililo na wananchama 20.
Aliyekuwa katibu mkuu msimamizi Moffat Kangi, John Ole Moyaki, Ibrahim Jillo Guyo, Richard Kirundi, Elizabeth Mueni na Roseline Odede watakuwa sehemu ya jopokazi hilo.Wengine ni ; Joash Odhiambo Dache, Doreen Muthaura, Albert Mwenda, Terry Chebet Maina, Hassan Sheikh Mohamed, Capt. (Rtd.) Simiyu Werunga, Mutuma Ruteere , Anne Ireri, Stephen Kayongo, Jafaar Mohamed, Sammy Chepkwony na Khadija Mire.
Omwanza Ombati, Joy Mdivo Masinde, Rosemary Kamau watahudumu kama makatibu wa jopokazi hilo kwa pamoja.
Jopokazi hilo linatarajiwa kuchunguza na kutambua changamoto za kisera,kisheria,usimamizi kati ya nyingine zinazotatiza utoaji huduma bora kwa polisi na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuzitatua changamoto hizo.
Aidha jopokazi hilo linahitajika kutathimini na kutoa mapendekezo kuhusu kuimarisha mazingira ya utenda kazi kwa polisi katika vitengo vyote sawa na maswala yote yanayosababisha idara ya polisi kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.