Mfumo wa E-FILING WAZINDULIWA

Jaji Mkuu humu nchini Bi. Martha Koome, amezindua rasmi mfumo wa kidijitali katika idara ya mahakama, unaokusudiwa kutumika katika usajili wa kesi, uhifadhi wa taarifa, na rekodi za kesi mbalimbali nchini.

Mfumo huu umepokelewa vyema na washikadau wa sekta ya mahakama, wakiuona kama hatua muhimu katika kuboresha utendaji wa idara ya haki ncini na kupunguza msongamano wa kesi mahakamani.

YouTube player

Katika mfumo huu wa kidijitali, washikadau wote, ndani na nje ya mahakama, wataweza kusajili kesi za aina mbalimbali kutoka popote walipo na kufuatilia maendeleo ya kesi kwa kuchunguza nyaraka za mahakama, ikiwa ni pamoja na hukumu na maamuzi ya mahakimu na majaji.

SOMA PIA | JSC Yachapisha Majina ya 7 Wanaowania Wadhifa wa Msajili Mkuu wa Mahakama.

Jaji Mkuu ameelezea mfumo huo kama hatua ya kihistoria kwa idara ya haki nchini Kenya na amesifu juhudi zilizowekwa katika kuuboresha mfumo huo ambao umetengenezewa humu nchini, akisema utawapa raia wa Kenya fursa ya kufuatilia takwimu za kesi zilizoko mahakamani kwa urahisi.

March 11, 2024