Marubani wa shirika la ndege la Kenya Airways wanatarajiwa kurejea kazini asubuhi ya kesho ( Jumatano 9.11.2022 Saa kumi na mbili asubuhi), baada ya mahakama ya leba kuwaagiza kusitisha mgomo huo na kurejea kazini.
Marubani wa KQ wamekua katika mgomo kwa muda wa siku nne, wakilalamikia kuondeolea kwa mpango wa malipo ya uzeeni pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi, mgomo ambao umesababishia kampuni ya shirika la KQ hasara ya mamilioni ya pesa, na mizigo ya thamani kuharibika kwa kuoza.
Shirika hilo la kitaifa lilikuwa limewasilisha mashtaka dhidi ya marubani hao waliogoma kwa kususia kazi tangu Jumamosi licha ya kuwa na agizo la mahakama dhidi ya kuandaa mgomo. Mahakama la leba aidha imetaka usimamizi wa shirika la Kenya Airways kutowachukulia hatua zozote za kinidhamu wmarubani hao wanaporejea kazini.