BY ISAYA BURUGU 17TH JULY 2023-Mary Wanyonyi ameapisha rasmi kama mwenyekiti mpya wa tume ya ugavi wa mapato nchini.

Jaji mkuu Martha Koome ameongoza hafla ya kuapishwa kwa Bi Wanyonyi anayekuwa mwenyekiti wa tatu wa tume hiyo.

Anachukua wadhifa huo kutoka kwa Jane Kiringai aliyestaafu mwezi Feburuari mwaka huu.

Rais  Ruto alimteua Bi  Wanyonyi kama mwenyekiti wa tume ya ugavi wa mapato  mnamo mwezi Mei mwaka huu wadhifa iliyokuwa ukigombaniwa  pia na  Thomas Ludindi Mwadeghu na Felicity Nkirote Biriri.

 

 

July 17, 2023