BY ISAYA BURUGU 21ST JUNE 2023-Maseneta wa mungano wa Azimio la umoja One Kenya wameondoka kwenye majengo ya bunge hilo baada wa ya spika kukosa kuidhinisha hoja ya kumhoji waziri wa kiviwanda moses Kuria kutokana na mashambulizi yake dhidi ya vyombo vya Habari.

Maseneta hao wamepinga hatua ya spika Amason Jeffa Kingi kutoruhusu  kuhojiwa kwa Waziri Kuria kutokana na kile wanachosema ni Waziri huyo kukosa uwezo na maadili ya kuendelea kuwa Waziri.Maseneta hao wanasema ni sharti katiba kubadilishwa ili kuruhusu Waziri huyo kufika mbele yao na wala sio utaratibu wa bunge la seneti unaopaswa kufanyiwa marekebisho.

Wameongeza kuwa iwapo Waziri Kuria ataruhusiwa kuhojiwa na seneti itakuwa ni sawa  na kusafisha mwenendo wake wanaosema unakiuka maadili

Katika siku za hivi karibuni ,Waziri kuria amejipata kwenye shutuma kutoka kwa wanachi wa tabaka mbali mbali,kuhusu  matamshi yenye matusi ambayo amekuwa akiyatoa haswa kuyaelekezea kwa vyombo vya Habari yanadhihirisha kuwa hapaswi kushikilia ofisi ya umma.

 

 

June 21, 2023