BY ISAYA BURUGU,28TH FEB,2023-Mgombea wa Urais wa chama tawala nchini Nigeria, Bola Tinubu anaongoza kwa kura katika majimbo 20 kati ya 36 nchini Nigeria.Matokeo hayo ya awali ni kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliokusanywa na shirika la habari la la Uingereza Reuters. Lakini wapinzani wamelisusia zoezi la kuhesabu kura kwa kuonesha mashaka ya vitendo vya udanganyifu.

Matokeo ya awali kwa majumuisho kwa ngazi ya majimbo kutoka kwa tume ya uchaguzi yanaonesha Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) yuko mbele kwa kura aslimia 39.7 sawa na milioni 5.4, dhidi ya Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha People’s Democratic Party (PDP) akiwa na kiasi cha kura milioni 4.4.sawa na asilimia 32.2.

Mgombea ambae anaonekana kama katokea nje kabisa katika wigo wa siasa wa Nigeria Peter Obi wa chama kidogo cha Labour anashika nafasi ya tatu kwa kura milioni 2.2 ikiwa sawa na asilimia 16.3Takriban zaidi ya thuluthi mbili ya idadi jumla ya kura kwa taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu bado haijatangazwa.

Lakini ushindi katika jimbo la Lagos – kwa kura 582,454 dhidi ya 572,606 kwa Tinubu imekuwa hatua kubwa kwa kwa Obi, ambe ameonesha kwa wagombea kutoka kambi mbili za muda mrefu ambazo zimkuwa zikipishana katika kuongoza taifa hilo tangu kumalizika kwa utawala wa jeshi mwaka 1999.

 

February 28, 2023