Ripoti ya mwaka wa 2024 kuhusu hali ya matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini imefichua kuwa kuna ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya vyuoni.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua ripoti hiyo katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi, afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya kupambana na mihadarati nchini NCADA Dkt. Anthony Omerikwa, alisema kuwa Pombe ndio inatumiwa zaidi na wanafunzi wa vyuo vikuu kwa [87pc], sigara inafuata kwa 64pc na shisha kwa 41.

Ripoti hiyo vilevile ilifichua kwamba wazazi na walimu ni miongoni mwa vyanzo vya msingi vya matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

February 13, 2025