BY ISAYA BURUGU 12TH JULY 2023-Maafisa wa Polisi wameanzisha  uchuguzi kufuatia kuawa kwa  kina mama wawili eneo la Ntulele Narok mashariki  ambao ni wafanyibiashara .Miili ya wawili hao inaripotiwa  kutupwa katika shamba la Kedong Narok mashariki.

Kamanda wa polisi kaunti ya Narok Kizito Mutoro akithibitisha kisa hicho amesema wawili hao walipigiwa simu na watu wanaodai ni wafanyibiashara wa maharagwe eneo la Ololulunga Narok kusini kabla ya  miili yao kupatikana imetupwa katika eneo la Kedong Narok mashariki.

Hadi kufikia sasa  hakuna aliyekamatwa kufuatia tukio hilo  .wakaazi wa eneo hilo wameonyesha ghadhabu yao huku wakitaja mauji hayo kuwa kitendo cha  kinyama na cha kuhuzunisha.

July 12, 2023