Makenzi

Mawakili wawili kati ya watatu waliokuwa wakimwakilisha mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie na washtakiwa wenzake wamejiondoa katika kesi inayoendelea katika Mahakama ya Shanzu.

Wawili hao George Kariuki na Elisha Komora, wamesema kuwa uamuzi wao wa kujiondoa katika kesi hiyo umetokana kukatishwa tamaa na idara mbalimbali za serikali katika kushughulikia kesi ya wateja wao. Mawakili hao waliyasema haya katika kikao na waandishi wa habari wakieleza kwamba maafisa wa polisi wamekuwa wakiwapa vijisababu kwa kukataa kumpa mteja wao mazingira mazuri.

Wakili wa tatu Wycliff Makasembo hata hivyo ameshikilia kwamba ataendelea kuwawakilisha Makenzi na wenzake, akimtaka Hakimu mkuu wa mahakama ya Shanzu jijini Mombasa Yusuf Shikanda kujiepusha na kupata shinikizo lolote linalojaribu kudhibiti mkondo wa kesi hiyo.

 

June 14, 2023