Mawaziri wateule

Mawaziri wawili walioteuliwa hivi karibuni na Rais William Ruto, Geoffrey Ruku (Waziri wa Utumishi wa Umma) na Hanna Cheptumo (Waziri wa Jinsia), wanatarajiwa kufanyiwa mchakato wa kupigwa msasa na kuhojiwa na Bunge la Kitaifa tarehe 14 Aprili 2025.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Karani wa Bunge la Taifa, Samuel Njoroge, shughuli hiyo itaendeshwa na Kamati ya Uteuzi ya Bunge, ambayo baada ya kuhoji wateule hao, itawasilisha ripoti yake bungeni kwa ajili ya hatua zaidi.

Wawili hao walichaguliwa mwezi uliopita kufuatia mabadiliko yaliyofanywa katika Baraza la Mawaziri na Rais Ruto.

SOMA PIA: Justin Muturi afutwa kazi kama waziri wa utumishi wa umma.

Wakati huohuo, Karani huyo wa Bunge amewaalika wananchi kuwasilisha maoni yao kuhusu ufaafu wa wawili hao kuhudumu katika nyadhifa walizopendekezwa. Maoni hayo yanatakiwa kuwasilishwa kufikia tarehe 10 Aprili 2025, saa kumi na moja jioni.

April 4, 2025

Leave a Comment