Kamati ya kitaifa inayoongoza mazungumzo ya pande mbili kati ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja, imeendelea na vikao vyake kuanzia asubuhi ya leo katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi, huku washikadau kutoka sekta mbalimbali wakiendelea kuwasilisha mapendekezo yao mbele ya kamati hiyo.

Mapema leo, Chama cha Mawakili nchini LSK kiliwasilisha mapendekezo yao kuhusiana na masuala ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na pia uundaji wa tume ya uchaguzi humu nchini. Katika mawasilisho yake, Mwenyekiti wa LSK Eric Theuri amependekeza kufanyiwa uhakiki kwa mitambo ya uchaguzi mkuu uliopita ili kuondoa shauku na pia haja ya kukamilisha mchakato wa uundaji wa tume ya uchaguzi nchini IEBC mapema.

September 26, 2023