Mizozo ya ndani katika chama cha Jubilee imeendelea kukithiri baada ya mrengo unaoongozwa na mbunge wa EALA Kanini Kega kumteua mbunge maalum Sabina Chege kama kaimu kiongozi wa chama.
Mbunge huyo mteule anachukua nafasi ya aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye alitimuliwa wakati wa mkutano wa Baraza la chama hicho ulilofanyika Jumanne asubuhi.
Kega ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu alisema uamuzi huo umeidhinishwa na wajumbe 22 kati ya 28 waliohudhuria mkutano huo.
Wanachama hao pia waliridhia maazimio mengine ambayo ni wazi yangezidisha vita kati ya pande zinazozozana.
Jubilee Party NEC issues the following statement. pic.twitter.com/dMqUEzmVwo
— Kanini Kega, CBS (@kaninikega1) May 2, 2023