BY ISAYA BURUGU,20TH MARCH,2023-Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi na seneta wa Kilifi Stewart Madzayo wamekamatwa jijini Nairobi katika mandamano ya Azimio yanayoendelea.
Mandamano hayo yameandaliwa kupinga kupanda kwa gharama ya Maisha.Taarifa zasema kuwa wawili hao walikamatwa katika jumba la mikutano la KICC ambapo walikuwa wamejiunga na wandamanaji wengine akiwema seneta Edwin Sifuna.Idadi isiyojulikana ya wandamaji pia wamekamatwa katika maeneo mbali mbali jijini huku polisi wakijizatiti kuzima mandamano hayo.
Maafisa wa polisi walilazimika kufyatua vitao machozi kuwatawanya wandamanaji hao.Mandamano makubwa na makabiliano yameshuhudiwa eneo la kibra ambapo wakaazi wameonekana wakiwarushia polisi mawe huku polisi wakijibu kwa kurusha vitao machozi.Wakati haya yakifanyika barabara zote za kuelekea ikulu zimesalia kuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
RIPOTI YA UN