Babu Owino Maandamano

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, amefikishwa mahakamani alasiri ya Alhamisi baada ya kuzuiliwa kwa muda wa yapata saa 48 na maafisa wa polisi.

Mbunge huyo alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumanne usiku na kushtakiwa kwa makosa kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupuuza mamlaka ya idara za serikali na kuhusika katika maandalizi ya maandamano ya upinzani yaliyofanyika jana.

Mawakili wa Babu Owino wameeleza kuwa upande wa mashtaka haukumfahamisha mteja wao sababu za kukamatwa na kuzuiliwa kwake, jambo ambalo wameushtumu kama kukiuka haki za kisheria za mbunge huyo.

Baada ya kukamatwa, mbunge huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Wang’uru katika eneo la Mwea, Kaunti ya Kirinyaga, ambapo inasemekana amekuwa akizuiliwa. Leo mchana, alisafirishwa hadi Makao Makuu ya Polisi wa Trafiki katika eneo la Nairobi baada ya wanafamilia na mawakili wake kuvamia kituo cha Wang’uru wakitaka aachiliwe.

 

 

July 20, 2023