BY ISAYA BURUGU 13TH JULY 2023-Mbunge wa eneo bunge la Mavoko  Patrick Makau amekamatwa. Makau amekamatwa nyumbani kwake Karen Nairobi asubuhi ya leo.

Nyumba ya mbunge huyo ilivamiwa mwendo was aa kumi za alfajiri na makachero kutoka kitengo cha upelelezi wa jinai DCI  waliompeleka katika afisi zao zilizoko Barabara ya Kiambu.

Kukamatwa kwa Makau kunahusiana na mandamano yaliyopelekea uharibifu mkubwa katika Barabara ya Nairobi Expressway  eneo la  Mlolongo  wakati wa mandamano ya kupinga serikali yaliyoitishwa na upinzani  jana kupinga gharama ya juu ya kimaisha.

Angalu watu tisa waliripotiwa kuawa wakati wa mandamano hayo  wakiwemo wanne kutoka Mlolongo,wawili kutoka Kitengela na mmoja kule EMali kaunti ya Makueni.

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki  amemlaumu kinara wa upinznai raila Odinga  kwa kuwa mwanzilishi wa vitendo vya ukiukaji sheria.

 

 

 

 

 

July 13, 2023