BY ISAYA BURUGU,18TH NOV 2022-Mbunge wa eneo bunge la Sirisia John Waluke ameachiliwa kwa dhaman aya shilingi milioni kumi pesa taslim na mahakama ya rufaa kusubiri kusikilizwa kwa rufaa aliyowasilisha dhidi ya hukumu yake ya miaka 67.Haya yanajiri baada ya Waluke mwezi jana kuwasilisha rufaa dhidi ya hukumu hiyo aliyopewa na mahakama kuu aikitaja kuwa kali muno na isiyohitajika.Hukumu ya mbunge huyo ilifuatia kesi ya ufisadi dhidi yake ambapo anatuhumiwa kuilaghai bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB shilingi milioni 313.Mbunge huyo alishatakiwa Pamoja na Grace Sarapay Wakhungu na kampuni ya Erad Supplies & General Contracts Limited (Erad); kampuni ambayo wawili hao ni wana hisa.Waluke na Wakhungu, kupitia kwa kampuni hiyo walipaswa kusambaza mahindi tani alfu 40,00 kwa bodi ya NCPB mwaka 2004 lakini wakatia mfukoni shilingi milioni 313 bila kusambaza mahindi hayo.