BY ISAYA BURUGU 29TH MARCH,2023-Chama cha ODM hivi leo kimemuandaikia barua spika wa bunge la kaunti ya Migori kuhusu ukosefu wa imani yake kwa baadhi ya wabunge wa bunge hilo.Wabunge hao ni 1. Hon. George Okinyi Omamba – ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya afya na mwakilishi wadi wa North  Kanyamkago).2Hon. Eunice Odii-  ambaye ni mwanachama wa jopo la spik ana mwakilsihi wadi wa ( Central Kanyamkago) 3. Hon. Norman Ogolla – ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya elimu  na MCA wa  East Kanyamkago) .4. Hon. Samson Olima Obonyo- ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maji na kawi na MCA wa  North Kadem).

Kufuatia  mawasiliano kutoka kwa spika hivi leo,wanachama wa jopo kazi la spika pia wamebadilishwa kama ifuatavyo:1. Hon. Eunice Odii- -mahala pake kuchukuliwa na  Hon. Philisters Makabong’o.2. Hon. Osewe Collince (North Kamagambo)  mahala pake kuchukuliwa na  Hon. Moses Magwe (Tagare).

Kwingineko wanachama wa kamati ya haki na maswala ya kisheria wamemwandikia spika wakidai  kuwa hawana Imani na mwenyekiti wao wa sasa  . Peter Mijungu ambaye ni MCA wa West Kanyamkago na hivyo basi wameanza kukusanya sahihi  kumwondoa. Haya yamejiri  wakati  watu wasiojulikana walivamia  bunge la kaunti ya Migori  kwa lengo la kuwavamia  wabunge wa bunge hilo waliohudhuria hafla  ya rais Wiliamu Ruto  mwishoni mwa juma kama ilivyodhibitishwa na kamanda wa polisi wa Migori Mark Wanjala.

.Aidha Wanjala amesema kuwa baadhi ya MCA walijeruhiwa  na tayari wamesha andikisha taarifa kuhusiana na kisa hicho.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

March 29, 2023