Mchungaji Ezekiel Odero amekata rufaa kufuatia hatua ya kufitiliwa mbali kwa usajili wa kanisa lake la New life international centre na msajili wa mashirika nchini.

Bw.Odero anasema kuwa hatua ya Serikali kufutilia usajili wa kanisa lake ni kinyume cha sheria na inapaswa kuangaziwa.

Kupitia mawakili wake, mchungaji huyo anamtaka Mwanasheria Mkuu kushughulikia suala hilo ndani ya siku 90 kuanzia leo.

Vilevile ameeleza kuwa kanisa lake litaendeleza shuguli zake huku wakisubiri mawasiliano ya mwanasheria mkuu. Makanisa mengine ambayo usajili umefutiliwa mbali ni pamoja na Goodnews International lake mchungaji Paul Mckenzie,Helicopter of Christ Church,Kanisa la Theophilus pamoja na Kanisa la Kings Outreach.

Wito wa kudhibiti makanisa umekuwa ukiongezeka huku Naibu Rais Rigathi Gachagua akiwataka viongozi wa kidini kuunga mkono mpango wa serikali wa kukagua kanuni zinazosimamia mashirika ya kidini.

Wito huu unajiri hasa baada ya vifo vya halaiki kushuhudiwa katika eneo la Shakahola.

August 18, 2023