Baraza la vyombo vya Habari nchini MCK limewakashifu maafisa wa polisi kwa kuwafungia nje wanahabari waliokuwa wakiripoti mkasa wa Shakahola.

Katika taarifa, MCK ilisema hatua hiyo inavinyima vyombo vya habari fursa ya kuripoti kuhusu suala la maslahi ya umma.Siku ya Jumatano, wanahabari walizuiliwa kwenda kwenye Msitu wa Shakahola na polisi.

Ardhi hiyo ya ekari 800 inamilikiwa na Mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International Church.

Mackenzie anashukiwa kuwafundisha wafuasi wa kanisa lake kufunga hadi kufa kwa imani ya kupaa mbinguni kukutana na Yesu Kristo.

April 27, 2023